Deuteronomy 5:4-9

4 a Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 5 b(Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

6 c“Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
7 dUsiwe na miungu mingine ila mimi.
8 eUsijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. 9 fUsivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mwenyezi Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Copyright information for SwhKC